Tuesday, February 28, 2017

Nokia 3310 yazinduliwa upya katika mfumo na mwonekano mpya

Kampuni ya simu ya Nokia imezindua upya simu aina ya nokia 3310 ambayo kwa sasa inakuja na muonekano mpya ambao unavutia zaidi kioo cha rangi yebye kuweza kuonekana vizuri kwa watumiaji wake.




Aidha simu hii ina uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa mwezi mmoja bila kuchaji, betri yake imeingezewa ubora ili kuweza kukidhi mahitaji ya watumiaji wake ambao mara nyingi watu hutamani kukaa na simu inayodumu na chaji kwa muda mrefu.

Pia simu hii imekuja na mchezo wa nyoka au snake xenzia game ambo ni maarufu kwa sinu nyingi za nokia.
Simu hii ina ukubwa wa kioo cha 2.4inch
Ina teknolojia ya 2G kwa ajili ya mtandao
Ina camera ya 2MP
Teknolojia ya bluetooth 3.0
Ina radio ya FM
Pia ina weza kucheza miziki katika mfumo wa MP3
Ina uwezo wa kufihadhi data mpaka 16MB
Na pia inasehemu ya kuweka memory card mpaka 32GB

Simu hii itapatikana kwa gharama ya Euro49 zaidi ya Tsh. 120,000/-


Like page yetu kwa habari zaidi @abgonlineTv
Abg OnlineTv
+255659570630
+255659445425
+255714007330

No comments:

Post a Comment