Friday, March 3, 2017

UBATIZO MKUBWA WAFANYIKA TANZANIA.

ABG ONLINETV.


Ubatizo mkubwa wa kihistoria umefanyika leo Tar 03.03.2017,nchini Tanzania jijini Mwanza katika Hotel yenye hadhi ya Kimataifa ijulikanayo kwa jina la VICTORIA PALACE HOTEL, ambapo watu zaidi ya 800 wamebatizwa.

Ubatizo huo nimatokeo ya mahubiri makubwa ya julikanayo kama USHINDI HATIMAYE yanayoendelea jijini mwanza ambayo yanaendeshwa na kanisa la waadventista wasabato kupitia chama cha wanataaluma na wajasiriamali (ATAPE), ambapo mafundisho mbalimbali ya neno la MUNGU yamekua yamekua yakitolewa.



Katika mahubiri hayo mpaka sasa watu zaidi ya 5,000 wamebatizwa kwa maji mengi na wengine wanaendelea kubatizwa, sambamba na hilo wachungaji watatu wa madhehebu tofauti wamemkiri yesu na kubatizwa kwa maji Mengi na kujiunga na kanisa la waadventistwa wasabato ulimwenguni.

Mahubiri hayo yanatarajiwa kuhitimishwa leo katika kanisa la waadventista wasabato MABATINI mwanza.

 



''MWANZA 2017---- USHINDI HATIMAYE''

 Lile page yetu kwa habari mbalimbali@AbgOnlineTv
+255659570630
+255659445425
+255714007330

No comments:

Post a Comment