Tuesday, February 28, 2017

MAFUA YA NGURUWE YASHAMBULIA MAGHARIBI MWA TANZANIA


ABG ONLINETV.


Mlipuko wa homa ya mafua ya nguruwe walikumba eneo la magharibi mwa Tanzania

Mlipuko wa ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe umeikumba wilaya ya Kalambo mkoa Rukwa kusini magharibi mwa Tanzania, na kusababisha vifo vya nguruwe karibu 200.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Bibi Julieth Binyura amesema serikali imepiga marufuku biashara ya nyama hiyo, na usafirishaji wa nguruwe hai ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo. Bibi Binyura pia amesema wanavijiji wa wilaya hiyo wamearifiwa kuhusu ugonjwa huo. Ofisa mifugo wa Wilaya hiyo Bw Wilbrod Kansapa amesema nguruwe wanaoonekana wakirandaranda wanakamatwa.

Ufugaji wa nguruwe unaendelea kuongezeka katika maeneo ya magharibi mwa Tanzania, kutokana na mahitaji makubwa kwenye miji mikubwa kama Dar es salaam.

CHANZO: CRI KISWAHILI

 
 UGONJWA WA MAFUA YA NGURUWE
  • Ni aina mpya ya homa inayosababishwa na virusi ambavyo ni rahisi kuambukizwa, na rahisi kuambukiza watu wengine.
  • Wagonjwa wa kwanza waliambukizwa mnamo April 2009 na ugonjwa huo umeenea upesi katika nchi nyingi duniani. 
DALILI ZAKE
Kama wewe au ndugu yako ana homa au ongezeko la joto la mwili
(zaidi ya 38°C / 100.4°F) na unaweza kuwa na mafua ya nguruwe
kama una dalili mbili au zaidi zifuatazo:
  • uchovu ambao sio wa kawaida
  • kuumwa kichwa
  • kuwa na mafua
  • maumivu ya koo
  • kushindwa kupumua na kukohoa
  • kukosa hamu ya kula
  • maumivu ya misuli
  • kuharisha na kutapika
JINSI UNAVYOSAMBAZWA  
Watu wenye homa ya mafua ya nguruwe, wanasambaza virusi kwa njia ya kikohozi au chafya, na watu wengine wanavuta hewa yenye virusi. Virusi vinaweza kuishi katika mikono na sehemu zingine kwa zaidi ya masaa 24.
JINSI YA KUJIKINGA WEWE NA FAMILIA YAKO.
  1. Zuia mdomo na pua kwa kitambaa kisafi au karatasi laini wakati unapokohoa au kupiga chafya. 
  2. Tupa kitambaa kwenye pipa la taka baada ya kukitumia.
  3. Osha mikono yako na sabuni na maji au na sabuni ya mikono yenye dawa ya kuulia virusi mara kwa mara na safisha sehemu za juu kila mara ili kuua virusi.
  4. Wajue marafiki watakaokusaidia. Wanaweza kuwa jirani zako, marafiki au ndugu wanaoweza kukusaidia wakati unapoumwa. Kwa mfano, wanaweza kwenda kukuchukulia dawa na chakula.
  5.  Kama wewe ni muomba hifadhi na una homa ya mafua ya nguruwe, wewe au rafiki yako ni lazima kuwasiliana na mfanyakazi wa Idara ya Uhamiaji (United Kingdom Border Agency) anayesimamia kesi yako ili wafanye mpango mwingine wakuchukua pesa zako za ruzuku, ili usiwe na haja ya kutoka mahali unapoishi. Ni lazima uwasiliane na msimamizi wa kesi yako au sehemu unayoripoti ili wafanye mipango mipya ya kuripoti.
  6. Kama ni mjamzito, endelea kufanya shughuli zako za kawaida, kama vile kwenda madukani, kutumia usafiri wa umma na kushiriki katika mikusanyiko ya kifamilia. Lakini ni vizuri kama hutawatembelea ndugu na marafiki wenye dalili za homa ya nguruwe. Kama unajua kwamba kuna wagonjwa wengi wanaoishi karibu na nyumbani kwako, ni vizuri kuepuka na mikusanyiko ya umati ya watu

Like page yetu kwa habari zaidi @abgonlineTv
Abg OnlineTv
+255659570630
+255659445425
+255714007330

1 comment:

  1. Slots - Dr. MCD
    Looking for 춘천 출장안마 Slot games to play 동두천 출장안마 in your home? At Dr.MCD, we offer you 청주 출장안마 the opportunity 전라북도 출장마사지 to 경기도 출장샵 play at our top-rated casinos, including Slots Vegas and

    ReplyDelete