Wednesday, October 19, 2016

INDIA:WATU 20 WAFARIKI DUNIA BAADA YA HOSPITALI KUUNGUA MOTO

Zaidi ya watu 20 wamekufa na wengine zaidi ya MIAMOJA kujeruhiwa nchini INDIA baada ya jengo la hospitali kushika moto Mashariki mwa nchi hiyo.


Mashuhuda wa tukio hilo wanasema moto huo ulianzia kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo ya Jimbo la ODISHA.

Wachunguzi wanasema umeme ni chanzo cha moto huo, watu wengi wamekufa kwa kuvuta moshi.

Mwaka 2011 watu 89 walikufa nchini INDIA baada ya moto kuzuka ghafla katika hospitali moja mashariki mwa mji wa KOLKATA.

Chanzo: www.tbc.go.tz

Endelea kua nasi :
abg-Onlinetv kwa habari za injili na kijamii
Contacts:
+255659570630
+255659445425




No comments:

Post a Comment