Na Amos Daniel (abgonline tv)
Je? umewahi fikiri jinsi watoto wanapokua na furaha na amani pindi wanaposikilizwa na watu wengi? Hii imejiri leo tarehe 30-7-2016 katika kanisa la waadventista wasabato Yombo, katika sabato ya wageni ya watoto iliyosimamiwa na idara ya watoto kanisani hapo, siku hiyo ilipendeza zaidi kwani watoto wengi walifurahi kujumuika na watoto wengine ambao si wa imani ya waadventista wasabato
Muhutubu katika sabato maalumu ya wageni ya watoto alikua Mwinjilisti Nick John Okech ambae pia ni mtoto mdogo kutoka katika kanisa la waadventista wasabato Yombo Dovya, mwinjilist Nick John Okech ana ndoto ya kuwa kama mchungaji Geofrey Mbwana ambaye ni makamu Raisi wa kanisa la waadventista wasabato ulimwenguni.
Mwinjilisti Nick John Okech alikua na somi lisemalo KUMTEGEMEA MWOKOZI ambalo somo hili lilijikita katika kitabu cha 1Samweli 7:3 na kuendelea, "kama wana wa Islael walivyomtegemea MUNGU
katika vita dhidi wa wafilisti na kuishinda vita hiyo ndivyo nadi twapaswa kumtegemea MUNGU na kushikamana nae nasi tutashinda katika Dunia hii ya taabu na magonjwa usiogope" alisema mwinjilist Nick John Okech
Pia aliongezea kuwa tegemeo letu lapaswa kujengwa juu ya MUNGU na si mwanadamu kwa maana Yeremia 17:5 linasihi kwa kusema kuwa amelaaniwa amtegemeae mwanadamu, pia wageni waliofika walipatiwa zawadi ya vitabu vya TUMAINI KUU ikiwa ni sehemu ya kusambaza ujumbe wa neno la MUNGU
Mchana mara baada ya kupata chakula watoto walionesha vipindi mbalimbali vilivyovutia waumini wote wakiofika katika siku hiyo maalumu, vipindi hivyo ni kama kukariri mafungu, uimbaji, na masomo ya misingi 28 ya kanisa la waadventista wasabato Duniani pia baadhi ya watoto walionesha kipaji cha kukariri mafungu marefu katika Biblia.
Kwa habari nyingi zaidi tembelea
www.facebook/abgonlinetv
Instagram:abgonlinetv
Youtube:abgonlinetv
twitter:abgonlinetv
email:abgonlinetv@gmail.com
Au kwa simu namba
+255 659 445 425
+255 659 570 630
+255 714 007 330
![]() |
Kulia ni mwinjilisti Nick John okech akiwa na wahubiri wenza waliomsindikiza katika sabato ya wageni |
No comments:
Post a Comment