Friday, October 21, 2016

KENYA:MSABATO AAPISHWA KUA JAJI MKUU


Na. ABG-ONLINETV

Jaji wa kiadventista msabato DAVID MARAGA aliye kataa kufanya kazi katika siku ya Sabato(jumamosi),ameapishwa rasmi na kua jaji mkuu katika nchi ya Kenya.


Katika ghafla ya kuapishwa kwake iliyofanyika katika ikulu ya Rasi wa Kenya Uhuru Kenyatta,Jaji DAVID MARAGA alimualika Rais wa kanisa la waadventista wa sabato Division ya Mashariki na kati Dr. BLASIOUS RUGURI kwaajili ya kumuombea kabla hajaanza utekelezaji wa majukumu yake mapya.


"Kama mkristo(mwadventista) niliadhimia kwamba kabla sijaanza mujukumu yangu mapya kama jaji mkuu nitamshukuru Mungu kwa kunifikisha sehemu hii ya Juu"Alisema Jaji mkuu David Maraga.


Dr.Blasious Ruguri alisema kua Jaji mkuu David Maraga ni mtu wa maombi na ni mfano wa kuigwa kwa waadventista wasabato wote.


Jaji mkuu David Maraga alisema kua itakua ni vigumu sana kwake kufanya kazi katika siku ya sabato(Jumamosi) na kwamba atamuweka Mungu mbele ya kazi yake.


Jaji mkuu David Maraga amechukua nafasi hiyo baada ya Aliye kua jaji mkuu kustaafu mwaka huu .

Chanzo:www.adventistreview.org


Abg-Onlinetv kwa habari za injili na kijamii.

Contacts:

+255659570630

+255659445425

No comments:

Post a Comment