Saturday, July 16, 2016

DAR ES SALAAM: MORNING STAR TV NA RADIO WASHEHEREKEA KUMBUKUMBU YA KUANZISHWA KWA VITUO HIVYO

Na Amos Daniel [ABG online TV]

Kituo cha utangazaji cha kanisa la waadventista wasabato Tanzania MORNING STAR TV na RADIO kilichopo Mikocheni B jijini Dar es salaam, hapo jana 15-7-2016 wameadhimisha miaka miwili ya kuanzishwa kwa Morning Star TV, na miaka kumi na tatu ya kuanzishwa kwa Morning star radio, maadhimisho hayo yalifanyika katika kanisa la waadventista wasabato Ushindi lililopo Mikocheni B jijii Dar es salaam, maadhimisho hayo yalipewa jina maalumu la USIKU WA SHUKRANI.

Sherehe hiyo ilisisindikizwa na waimbaji mbalimbali waliopata fursa ya kumtukuza MUNGU siku hiyo kama vile:- Angel Magoti, Light bearers na Gospel flames kutoka katika kanisa la waadventista wasabato Magomeni, pia watu mbalimbali walifika ili kushuhudia maadhisho hayo na ilirushwa live katika Morning star TV na Morning star radio

Mchungaji Steven Leta alikua ni mmoja kati ya wachungaji waliohudhuria katika maadhimisho hayo na kupata fursa ya kunenena na watu waliokuwa wakifatilia sherehe hiyo, ambapo alisisitiza watu kuzidi kumtegemea MUNGU katika mambo yote na kuwapa changamoto waumini wote kwa kusoma fungu kutoka katika Biblia lililotoka katika kitabu cha KUTOKA 20:8-11 fungu lilosisitiza watu kufanya kazi katika siku sita na kupumzika siku ya saba (Sabato), "Fungu hili MUNGU amewapa binadamu kama offer ili kupata pumziko la pekee ili kueka afya za binadamu sawa kwa maana kwa siku sita hujapata pumziko na hivyo MUNGU alitenga siku hiyo iwe ni ya mibaraka kwenu" alisema,

Pia taasisi ya The same quality foundation (SQF) inayoshughulika na matibubu mbalimbali ya magojwa, walitoa zawadi mbalimbali kwa mtangazaji wa Morning star TV na Radio Emmanuel Maduhu ambaye ni balozi wa taasisi hiyo, pia walitoa zawadi kwa maarafiki wa karibu wa Taasisi hiyo (SQF) Light bearers ambao wanashirikiana kwa pamoja katika huduma hiyo ya matibabu, pia walifanikiwa kutoa zawadi katika uongozi wa kituo cha Morning Star TV na Radio kama shukrani za dhati kwa ushirikiano walioonesha juu yao.

 
WAIMBAJI WA KIKUNDI CHA LIGHT BEARERS WAKIMTUKUZA MUNGU.

MWIMBAJI ANGEL MAGOTI AKIMTUKUZA MUNGU.
BAADHI YA WATU WALIOHUDHURIA
GOSPEL FLAMES KUTOKA MAGOMENI S.D.A CHURCH WAKIMTUKUZA MUNGU.
 
ZAWADI IKITOLEWA KWA MKURUGENZI WA LIGHT BEARERS. 

No comments:

Post a Comment