Thursday, August 25, 2016

BI HARUSI MTARAJIWA AKAMATWA AKIJARIBU KUTOA MIMBA



Na Amos Daniel

Operesheni maalumu ya kushtukiza iliyofanywa jana na askari nchini Uganda katika hospitali maarufu kwa utoaji mimba iitwayo Miriam medical centre na kuzuia shughuli za utoaji mimba katika hospitali hiyo

Katika msako huo walifanikiwa kukamata mwanafunzi aliyetaka kutoa mimba akiwa katika sare za shule, mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 15 aliwekwa chini ya ulinzi katika kituo cha kawempe

Pia alikutwa bibi harusi mtarajiwa aliyejulikana kwa jina la Jory ambae anatarajia kufunga ndoa jumamosi ya tarehe 27-08-2016 akitaka kutoa mimba ambayo alidai kuwa siyo ya mwanaume anayetarajia kuolewa nae bali ni ya mchepuko

Pia mmoja wa mabinti aliyekutwa akitokwa na damu nyingi sana baada ya kutolewa ujauzito na kukimbizwa haraka katika kituo cha afya cha Malago ili kuokoa maisha yake

Moses Kuwesa daktari mashuhuri wa shughuli ya utoaji mimba aliyekamatwa aliwaambia polisi kuwa kumtia nguvuni ni kummaliza kwani anaishi kwa kutegemea shughuli za utoaji mimba.

Jamii zetu hata hapa Tanzania imekumbwa na tatizo hili la utoaji wa mimba, ikumbukwe kuwa ni kinyume na Sheria ya Nchi, lakini pia ni dhambi mbele za Mungu.

Utoaji mimba ni kosa kubwa kisheria nchini Uganda na ukikamatwa na kuthibitika kuwa unafanya shughuli hiyo utapelekwa jela miaka 14.

Friday, August 19, 2016

Umekaribishwa Ufunge kambi la mtaa wa Yombo.

Usain Bolt-NayawezaYote katika Yeye Atutuaye Nguvu.

Kutoka Adventist Review
Mwanadamu mwenye spidi zaidi duniani, raia wa nchi ya Jamaica Usain Bolt mshindi medali ya dhahabu katika mashindano ya olimpiki huko Rio Brazil, ni kijana aliyelelewa katia famili ya waadventista wasabato japo yeye si mshiriki wa kanisa hilo, Usain Bolt amekuwa akisafiri biblia yake kila mahali anapokwenda, iko siri zaidi ya ushindi anayotumia Usain Bolt nayo ni kumtegemea Mungu, sio tu kwa kufanya mazoezi pekee bali kusoma neno lake na maombi.

Nasi tuna nafasi ya kusaidia jamii inayotuzunguka kumtumainia Mungu katika maisha yao ya kila siku.