Kufuatia kuandama kwa mwezi, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM limetoa tahadahari kwa wakazi wa Mkoa wa huo katika kipindi cha Sikukuu ya EID EL FITR kuwa makini na kujiepusha na matukio ambayo yanaweza kuharatisha maisha.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM Kamishna wa Polisi SIMON SIRRO amesema jeshi hilo limejipanga kukabiliana na matukio mbalimbali na kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya ibada.
Kamanda SIRRO ametoa tahadhari kwa wamiliki na waendeshao vyombo vya moto kuepuka kukodisha magari yao kwa watu wasiowajua.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi limewakamata watu 400 wanaotuhumiwa kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu pamoja na kupata silaha iliyotengenezwa kienyeji katika eneo la MBURAHATI BARAFU wakati wa msako uliofanywa na jeshi hilo.
SOURCE TBC.
No comments:
Post a Comment