Tuesday, July 5, 2016

MAADHIMISHO YA JUBILII YA MIAKA 50 YA KANISA LA SDA KIRUMBA YAFANA.

Kanisa la waadventista Wa sabato la Kirumba jijini Mwanza, siku ya sabato ya tarehe 2/7/2016 na 3/7/2016 ni siku ambazo walikuwa wakihitimisha maadhimisho ya miaka 50 ya kuazishwa kwa kazi ya injili katika jiji la Mwanza.

Maadhimisho hayo yalifayika katika uwanja wa CCM kirumba ulijumuisha makanisa karibu yote ya jiji la Mwanza huku wachungaji toka katika mji,bo makuu yote mawili, Jimbo kuu la Tanzania kusini na kaskazini kuhudhuria, pamoja na wachungaji Wastaafu waliowahi kulitumikia kanisa la Kirumba walikuwepo.

wakizungumza kwa nyakati tofauti, wachungaji hao wamemshukuru Mungu kwa Miaka 50 kwani imeleta mageuzi makubwa ya ijnili toka kuwa na kanisa moja mpaka kufikia zaidi ya makanisa 85 yaliyopo sasa hivi jijini Mwanza.

Pia familia za washiriki wa kwanza kabisa katika kuazisha kanisa hilo, walipata nafasi Kutoa shuhuda mabli jinsi walivyoona mkono wa Mungu tangu kuanziashwa kwa kanisa hilo hadi hivi leo, Familia ya Mzee Lazaro Bomani wakiongozwa na Jaji mstaafu ndugu Bomani, walielezea namna baba yao Mzee Lazaro alivyojitolea kununua kiwanja yeye pamoja na familia ya Mzee Kazi.

Siku ya Jumapili maadhimisho hya yalifungwa na Mhe. Hamisi Kigwangala. akishuhudia gwaride zuri toka kwa vijana wakakamavu wa PFC na AC.



1 comment: